Ansarulllah imesema kuwa itatoa majibu makali kwa utawala wa Kizayuni kufuatia mauaji hayo na kuendelea vita na mauaji ya kimbari ya Tel Aviv katika Ukanda wa Gaza.
Dhaifallah al Shami mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah amesema kuwa tuna majibu ya kushangaza ambayo si rafiki wala adui anaweza kutarajia. hakuna rafiki wala adui angeweza kutarajia.
Kauli hiyo imetolewa saa chache baada ya jeshi la Yemen kufanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
Jeshi la Yemen jana lilitangaza kuwa limeishambulia meli ya Israel katika pwani ya Bahari Nyekundu kwa kutumia kombora la balistiki.
Msemaji wa jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema katika taarifa iliyorushwa na televisheni ya nchi hiyo kuwa meli ya Israel ya mafuta ya Scarlet Ray imelengwa kwa kombora la balistiki kaskazini mwa Bahari Nyekundu na kwamba jeshi la Yemen limefanikiwa kutimiza malengo yake katika oparesheni hiyo.
Ahmed Ghaleb al Rahawi Waziri Mkuu wa serikali ya umoja kwa ajili ya mabadiliko na katiba ya Yemen na maafisa wengine wanane waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel Alhamisi iliyopita huko Sana'a mji mkuu wa Yemen.
Abdul Malik al Houthi Kiongozi wa harakati ya Ansarullah amewasifu wahanga jinai hiyo ya Israel na kuwataja kuwa ni mashahidi wa Yemen yote nakulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni dhidi ya raia.
Your Comment